Klopp awachana akina Man City, Mourinho na Guardiola.

Jurgen Klopp.
Kuelekea mechi yao ya leo ya fainali ya kombe la Capital One, Kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amezungumza maneno ambayo kwa upande mwingine yanaonekana kuwa dhihaka kwa wapinzani wao wa leo Manchester City. Klopp amesema kuwa yeye haitaji kufundisha klabu yenye pesa nyingi ili kushinda vikombe, Klopp anasema kama pesa zipo sawa unatumia ila sio lazima upewe pesa nyingi za usajili ili ufanye vizuri. Kauli hiyo inaonekana kuwalenga makocha bora duniani kwa sasa yaani Jose Mourinho na Pep Guardiola ambao wote wamekuwa wakiwinda kufundisha vilabu vyenye pesa nyingi.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment