Louis Van Gaal asema Rooney atakuwa fiti.


Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United mholanzi Louis Van Gaal akiongea na waandishi wa habari ameelezea hali ya mchezaji wake nyota na pia kepteni wa timu hiyo Wayne Rooney, Kocha huyo anasema Rooney kwa sasa anavaa bandeji ngumu mguuni kwake ili kuepusha kujitonesha jeraha alilonalo na pia akisisitiza kuwa haitaji kufanyiwa upasuaji kwakuwa jeraha hilo ni dogo. Van Gaal amesema kuwa Rooney ataendelea kuwa nje kwa muda wa wiki mbili na nusu na mashabiki wa Uingereza wasiwe na wasiwasi kwa kuwa nyota huyo atacheza michuano ya Euro hapo mwezi wa sita lakini kabla ya kufikia huko bado Manchester United wanahitaji mchango wake.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment