 |
Lionel Messi dhidi ya Arsenal. |
Mchezaji bora wa dunia na mshambuliaji hatari wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amezungumza machache baada ya kutoka London ambako walicheza mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Arsenal na kushinda kwa mabao mawili kwa bila na mabao hayo yalifungwa na mchezaji huyo kutoka Argentina. Messi amesema kuwa amefurahishwa na ushindi walioupata ila akasema kuwa hawawezi kusema kuwa wamekwisha vuka kwenda kwenye hatua ya robo fainali kwa kuwa chochote chaweza kutokea kwenye mechi ya pili pale Nou Camp. Messi anasema Arsenal wana wachezaji wazuri wanaoweza kufanya mambo kuwa magumu kwa timu pinzani muda wowote wa mchezo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment