 |
Alexis Sanchez. |
Nyota wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Chile Alexis Sanchez amezungumzia mechi yao ya leo dhidi ya Manchester United. Sanchez alizungumzia mechi ya kwanza waliyokutana na Man U na kusema kuwa ile ndio mechi bora kwangu kucheza kwa msimu huu, anaendelea kwa kusema tuliingia uwanjani tukiwa na hasira ya kushinda na hata ukiangalia nyuso zetu wote utagundua ni nini tulikuwa tunataka. Sanchez anasema kama tunataka ubingwa ni lazima leo tushinde dhidi ya Manchester United japokuwa ni wagumu sana ila hakuna namna ni lazima tupambane sana ili tupate ushindi. Alexis Sanchez ni moja ya nyota wa Arsenal watakaokuwa uwanjani leo kupambana na Manchester United pale Old Trafford.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment