Vardy amtaja beki mgumu kuliko wote aliyekutana nae msimu huu.
-
Nyota wa klabu ya Leicester City Jamie Vardy akiwa ndiye mfungaji bora wa ligi ya Uingereza mpaka sasa ametoa mtazamo wake kuhusiana na beki mgumu kuliko wote ambaye amekutana nae msimu huu. Vardy amemtaja beki wa Manchester United Chris Smalling kuwa ndiye beki mgumu kuliko wote aliyekumbana nae msimu huu na kuongeza kuwa ukiwa unacheza dhidi ya Smalling una shughuli ngumu maana hakuachi popote uendapo uwanjani huwa yupo nyuma yako. Chris Smalling anatarajiwa kuukosa mchezo wa kesho kwa kukabiliwa na majeraha madogo.
0 comments:
Post a Comment