 |
Claudio Ranieri akisalimiana na Arsen Wenger. |
Kocha mkuu wa klabu ya Leicester City Claudio Ranieri akiongea na waandishi wa habari kuelekea kwenye mechi yao ya leo dhidi ya Arsenal amegusia mambo kadhaa ambayo kwa namna nyingine unaweza kusema ni kijembe kwa timu ya Arsenal. Claudio Ranieri amesema kuwa Arsenal wana presha sana na Wenger anajaribu kuwapa presha Leicester wakati timu yake ndio yenye presha maaana kwanza inatumia kiasi kikubwa cha pesa kila msimu wakati Leicester inatumia kiasi kidogo sana cha pesa, Pia Ranieri amesema Arsenal isipochukua ubingwa msimu huu itakuwa ni janga kubwa kwao kuwahi kutokea kwa siku za hivi karibuni. Leicester inangia uwanjani leo dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates majira ya saa tisa ikiwa na kumbukumbu ya kupigwa bao tano kwa mbili (5-2) mechi ya kwanza ikiwa uwanja wa nyumbani.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment