 |
Thierry Henry. |
Gwiji wa zamani wa klabu za Arsenal na FC Barcelona Thierry Henry amewapa Arsenal mbinu ya kuifunga timu yake ya zamani FC Barcelona na kama wasipofanya hivyo basi watakuwa wamekwisha. Henry amewaonya Arsenal kutocheza mpira unaofanana na Barcelona na pia amewataka kuzuia mashambulizi ya Barcelona kitimu na isiwe kazi ya mabeki wenyewe. Pia Henry amewaeleza Arsenal kuwa wajiandae kumiliki mpira kwa asilimia 30 tu na wafanye mashambulizi ya kushtukiza wakitumia mawinga wao huku pia wakirudi kusaidia mabeki wao wa pembeni. Thierry Henry ni mmoja wa wachezaji waliopoteza pambano la fainali dhidi ya FC Barcelona mwaka 2006.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment