 |
Arsen Wenger. |
Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Arsen Wenger akiongea na waandishi wa habari, amezungumzia mambo kadhaa kuhusiana na mwenendo wa klabu yake kwa sasa haswa kipindi hiki kigumu anachokabiliwa na ratiba ngumu. Wenger alimzungumzia nyota wa klabu hiyo Alexis Sanchez na kusema kuwa, juzi kwenye mechi ya FA dhidi ya Hull City hakuwa kwenye kiwango chake ila Jumanne kwenye mechi dhidi ya Barcelona kwa wasiomjua Alexis Sanchez ni nani basi watamjua siku hiyo, Pia Wenger amesema Arsenal hawatakuwa na nafasi nyingine ya kuifunga Barcelona zaidi ya hii ya sasa na inabidi waitumie nafasi hiyo vizuri, pamoja na hivyo Wenger amesema wamekuwa wakishinda ugenini mara nyingi kwenye UEFA lakini pia wamekuwa wakifungwa mara nyingi kwenye mechi za nyumbani jambo ambalo hawataliruhusu kwenye mechi hii dhidi ya Barcelona. Wenger amewaasa wachezaji wake kuwa na nidhamu muda wote wa mchezo na pia wabalance mchezo yaani wasikubali kushambuliwa muda wote pia wazuie kitimu.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment