Alan Shearer ataka Harry Kane awe chaguo la kwanza England.


Mfungaji bora wa muda wote wa ligi kuu ya Uingereza Alan Shearer amemtaka kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson kumpa nafasi ya kwanza mshambuliaji wa klabu ya Totenham Hotspur Harry Kane kwenye kikosi cha nchi hiyo kinachojiandaa na michuano ya Euro 2016. Alan Shearer amesema ubora wa Harry Kane mbele ya goli ni dhahiri anahitaji nafasi ya kipekee kwenye kikosi cha taifa na hadhani kama kuna mtu atabisha kuhusu hilo. Harry Kane anaongoza kwa ufungaji katika ligi kuu ya Uingereza akiwa na mabao 21 mawili ikiwa ameyafunga katika mechi iliyopita dhidi ya FC Bournemouth kwenye ushindi wa mabao matatu.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment