 |
Diego Costa. |
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na klabu za Liverpool na Atletico Madrid Luis Garcia amemtaka kocha wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque kumtumia mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa katika mashindano ya Euro 2016. Garcia amesisitiza kuwa Costa ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kuivusha timu kutoka sehemu moja kwenda nyingine, Pia akasisitiza kuwa Costa anatakiwa atumike kama mshambuliaji chaguo la kwanza. Garcia hakuishia hapo ila aligusia pia kuwa Isco anatakiwa katika kikosi hicho bila kukosa maana ana vitu vya ajabu ambavyo vinaweza kuisaidia timu. Diego Costa ameachwa kwenye kikosi kitakacho cheza mechi za kirafiki dhidi ya Italia na Romania kwa madai kuwa kocha wa timu ya taifa Vicente del Bosque hafurahishwi na nidhamu ya mchezaji huyo, ila Jumanne Del Bosque alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa amemuacha Costa kwa sababu ya majeraha madogomadogo aliyonayo.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment