Laurent Koscienly; Bado tuna uwezo wa kuchukua Ubingwa na Wenger ndiye mtu sahihi.


Beki wa kati wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa amesema bado wana matumaini ya kuchukua Ubingwa kutokana na ushindi walioupata mwisho wa wiki dhidi ya Everton. Koscienly anasema kucheeza mechi tatu mfululizo bila ushindi ndiko kulikopelekea matatizo yote ambayo kwa sasa yanawaweka mbali na ubingwa. Beki huyo kisiki amesema sasa mechi zimebaki nane na tumepanga kila mechi kucheza kama fainali ili kupata matokeo mazuri, kwaiyo mpaka sasa naweza kusema tuna fainali nane za kucheza, Pia Koscienly amejitetea kwa kusema wamesuasua kwa sababu ya wachezaji waliopata majeraha ya muda mrefu kama Carzola na Welbeck, na pia amesisitiza kuwa Wenger ni mtu sahihi kwa klabu hiyo na mashabiki hawapaswi kumbeza.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment