 |
Bale akiwa na mke wake. |
Mchezaji ghali kuliko wote duniani Gareth Bale ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, jana alifanikiwa kuufahamisha ulimwengu kuwa amepata mtoto wa kike. Bale aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuwa mwenza wake aitwaye Emma Rhys-Jones amejaliwa kujifungua mtoto wakike anayeitwa Nava Valentina Bale. Nava Valentina atakuwa ni mtoto wa pili wa Bale na mpenzi wake baada ya mwaka 2012 walipofanikiwa kumpata binti yao wa kwanza aitwaye Alba Violet. Bale hajaweza kujiunga na timu yake ya taifa inayojiandaa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Ireland kwa sababu alikua katika shughuli hiyo ya kifamilia.
 |
Bale na mtoto wake. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment