Don Balon yamchonganisha Ozil na Wenger.


Mtandao wa Don Balon leo umetoa taarifa za kushangaza zinazosema kuwa nyota wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil amepanga kuondoka klabuni hapo mwisho wa msimu kama kocha wake wa sasa ambaye ni Arsen Wenger ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo. Don Balon wanasema kuwa Ozil amekuwa akichoshwa na mbinu za kocha huyo ambazo zimekuwa zikiwafanya washindwe kushinda mataji ya muhimu katika klabu hiyo, Taarifa hizo ni njema kwa vilabu vya La Liga kama Atletico Madrid ambayo imekuwa ikitafuta mchezaji aina ya Ozil.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment