Iwobi atakiwa kuipiga chini Nigeria.

Alex Iwobi.
Kiungo wa klabu ya Arsenal Alex Iwobi ambaye alifunga kwenye mechi yake ya kwanza ya ligi dhidi ya Everton Jumamosi ametakiwa kukataa ofa ya kuchezea kikosi cha taifa cha Nigeria maarufu kwa jina la Super Eagles. Iwobi amekwisha kuiwakilisha England katika ngazi ya U16, U17 na U18 kabla ya kukubali kuitwa kwenye kikosi cha Nigeria ambako alicheza mechi mbili za kirafiki akiwa na timu hiyo. Iwobi ambaye ni mtoto wa dada yake na nguli wa soka barani Afrika Jay Jay Okocha bado hatma yake kisoka haijajulikana kwa kuwa bado hajaichezea Nigeria mechi ya mashindano yoyote zaidi ya mechi za kirafiki, huku hayo yakiendelea Daniel Amokachi amemtaja Iwobi kama moja ya wachezaji watakaoichezea Nigeria kwenye mashindano African Cup of Nations ambapo watakutana na Egypt na mechi ya kwanza ni Ijumaa. The Mirror limeripoti kuwa linategemea kuwa Iwobi atakataa ofa ya kujiunga na kikosi cha Nigeria ili aichezee England maisha yake yote kama hapo mwanzo alipokuwa na miaka 16.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment