 |
BBC. |
Baada ya jana kuipiga Sevilla jumla ya mabao manne huku nyota wake muhimu wakirudi kwenye ubora wao, Zidane ameamua kuipongeza timu yake na kusema kuwa Real Madrid kwa sasa imerudi kwenye ubora wake na wapo tayari kwa mechi kubwa kuliko zote kwenye ligi hiyo iliyopachikwa jina la "El Classico" ambayo huwakutanisha Real Madrid dhidi ya FC Barcelona. El Classico hii itakuwa ndiyo ya kwanza kwa kocha Zinedine Zidane tangu awe kocha mkuu wa klabu hiyo na itapigwa katika uwanja wa Nou Camp tarehe 2 April. Utamu wa mechi hiyo utaongezeka zaidi kwa kuwa makocha wa timu hizo mbili nao wameshawahi kuicheza mechi hiyo kila mmoja akiwa kwenye timu ambayo kwa sasa anaifundisha, Pia itawakutanisha wachezaji mahiri kila upande ukizingatia kwa sasa Real Madrid nyota wake wameshapona na wote wanategemewa kuwepo kwenye mechi hiyo (MSN vs BBC).
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment