Nyota watano Arsenal kupewa mikataba mipya.
-Imefahamika kuwa klabu ya Arsenal inajiandaa kuwapa nyota wake watano mikataba mipya ifikapo mwisho wa msimu huu. Gazeti la Times limedokeza kuwa Arsenal inajiandaa kutoa mikataba minono kwa nyota wake watano ambao ni Santiago Carzola ambaye anaingia miezi 12 ya mwisho kwenye mkataba wake, Mesut Ozil, Alexis Sanchez, Jack Wilshere na Alex Oxlaide-Chamberlain. Pia Arsenal bado hawajajua kama wampe mkataba mpya kepteni wa timu hiyo Per Mertersacker au wamwache, ila kwa hali inavyoonekana ni kwamba Mertersacker ataongezewa mkataba wa mwaka mmoja badala ya kuuzwa.
0 comments:
Post a Comment