Obama ashindwa kupanga ratiba ya watoto wake kuonana na Messi.
-Rais wa Marekani Barack Obama amesafiri na familia yake kuelekea nchini Argentina. Obama anasema amewapeleka watoto wake nchini humo ili wakaonane na watu maarufu duniani wanaotoka katika taifa hilo, Obama amesema watoto wake wameshaonana na baba mtakatifu wa kanisa la Roma Papa Francis na pia wangependa kuonana na mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ambaye nae yumo nchini humo na timu ya taifa wakijiandaa na michezo ya kirafiki lakini Obama amesema yeye hawezi kupanga ratiba hiyo. Obama amesema pia amewapeleka Sasha na Malia kuona namna mji wa Buenos Aires ulivyo mzuri.
0 comments:
Post a Comment