Beki wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya FC Barcelona Gerard Pique akiongea na waandishi wa habari kwenye kambi ya timu ya taifa ya Hispania amewataja washambuliaji watatu hatari aliowahi kukutana nao. Pique amemtaja Didie Drogba kuwa ni mmoja ya washambuliaji hatari zaidi duniani aliowahi kukutana nao, Pia Pique amemtaja Robert Lewandowski kuwa ni mmoja ya watu waliomsumbua sana katika soka wakati timu zao zilipokutana, Pique aliweka ushabiki pembeni na kuamua kusema ukweli kuwa Cristiano Ronaldo ni mmoja ya washambuliaji ambao akikutana nao huwa wanamnyima usingizi. Pique anafahamika kwa kutompenda kabisa Cristiano Ronaldo lakini jambo hilo halikumnyima yeye kutaja ubora wa Cristiano Ronaldo, Pique na Ronaldo watakutana mwezi wa nne tarehe mbili katika mechi ya "El Classico".
 |
Drogba dhidi ya Pique.
|
 |
Gerard Pique dhidi ya Robert Lewandowski. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment