Arsenal wampata mrithi wa Walcott kwa paundi milioni 25.
-Imeripotiwa na magazeti mengi ya ulaya siku ya leo kuwa Arsenal imepanga kumpiga bei mshambuliaji wake Theo Walcott na kumsajili mchezaji bora wa ligi hiyo kutoka barani Afrika katika nchi ya Algeria na si mwingine ni Riyad Mahrez. Imefahamika kuwa Arsenal imemfanya Mahrez kuwa namba moja katika orodha ya wachezaji inaowahitaji msimu ujao katika kikosi chao na mchezaji huyo wa Leicester City atapatikana kwa kiasi cha paundi milioni 25. Mahrez amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu. Walcott ameshindwa kuwika katika kikosi hicho kwa misimu kadhaa sasa na klabu hiyo imeona haitaweza kumvumilia kwa msimu mwingine.
0 comments:
Post a Comment