Mashabiki wa Arsenal wapanga kuongeza nguvu Jumamosi kwenye mechi dhidi ya Norwich.


Taarifa kutoka mtandao wa Goal.com unaeleza kuwa makundi ya mashabiki wa Arsenal wakiongozwa na kundi la "The Black scarf Movement" wataendelea kuonyesha mabango ya kuwataka Wenger na tajiri wa timu hiyo Stan Kroenke kuachia ngazi kwenye timu hiyo. Goal.com walimpata kiongozi wa "The Black scarf Movement" aitwaye Mark King, naye aliwataarifu kuwa kwenye mechi ya Jumamosi dhidi ya Norwich City pale Emirates, mashabiki watanyanyua mabango yanayosomeka ujumbe unaosema "Its Time for Change" yaani ni muda wa mabadiliko na mabango hayo yatanyanyuliwa dakika ya 12 na ya 78 ikiashiria miaka 12 bila ya ubingwa wa England. Arsenal wamefanikiwa kushinda mechi nne tu kati ya 13 walizocheza hivi karibuni na mashabiki wameamua kuanza kwenda kinyume nao maana wamechoshwa na mwenendo wa klabu yao.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment