Arsenal yamtolea £16m kiungo.


Taarifa ndani ya kalbu ya Arsenal zinadai kuwa klabu hiyo ipo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 16 kwa ajili ya kumnasa kiungo kutoka Crotia Marcelo Brozovich anayekipiga katika klabu ya Inter Milan. Brozovich (23) anaichezea Inter Milan kwa mkopo akitokea Dynamo Zagreb na anaingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Inter Milan, Na tayari jarida la Corriere dello Sport linalochapishwa na Daily Star limetaarifu kuwa upo uwezekano wa nyota huyo kutua Emirates. Arsenal wanahitaji kusajili viungo kutokana na viungo wao waliopo wengi miaka imeanza kuwatupa mkono kama Arteta na Flamini.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment