 |
Fernando Torres. |
Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Fernando Torres jana alifanikiwa kuvunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka akiwa na Liverpool, Torres jana aliisaidia klabu yake ya Atletico Madrid kupata ushindi muhimu wa bao moja kwa sifuri dhidi ya timu ngumu ya Athletic Bilbao, bao la jana la Torres linamfanya kuwa amefunga mabao kwenye mechi tano mfululizo na kuweka rekodi kwa kuwa hapo mwanzo alipokuwa na Liverpool aliishia kufunga mfululizo kwenye mechi nne tu. Wiki ijayo Torres atakuwa ni miongoni mwa washambuliaji wa Atletico watakaopambana na klabu ya Bayern Munich kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa (UEFA).
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment