Xhaka akubaliana na Arsenal maslahi binafsi.

Granit Xhaka.
Taarifa za awali zinadai kuwa kiungo wa timu ya taifa ya Uswiss na klabu ya Borrusia Monchengladbach ya Ujerumani Granit Xhaka ambaye amekuwa akihusishwa na klabu ya Arsenal kwa muda mrefu sasa wamefikia makubaliano ya awali na klabu hiyo ya London. Xhaka ni mchezaji ambaye ameshindwa kuficha hisia zake juu ya kujiunga na klabu ya Arsenal na pia kocha wa klabu hiyo anafahamika kwa kuvutiwa zaidi na kiungo huyo ambaye thamani yake inatajwa kuwa paundi milioni 34. Mtandao wa Bleacher Report amesema kuwa mazungumzo baina ya pande mbili yanaendelea na yanaonyesha matumaini ya dili hilo kukamilika mwanzoni kabisa mwa kipindi cha usajili.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment