Bale aweka wazi kuhusu Ronaldo.
-Mchezaji bei ghali zaidi duniani Gareth Bale amesema yeye na mchezaji mwenzake Cristiano Ronaldo hawana shida kama inavyosemekana na vyombo vingi vya habari, Bale amesema yeye na Ronaldo wanaelewana sana na kila mmoja anaangalia namna ya kuisaidia timu yao ipate kombe msimu huu, Bale aliiwezesha timu yake kupata ushindi mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Rayo Vallecano ambayo ilitangulia kwa kufunga mabao mawili ya haraka kipindi cha kwanza, Pia Bale anasema Cristiano ni moja ya watu wazuri aliowahi kukutana nao maana kwanza alianza kwa kumsaidia kutafsiri lugha ya kihispaniola kwa kiingereza alivyosajiliwa na Real Madrid. Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wanatarajiwa kuungana kesho kwenye mchezo utakaowakutanisha na Manchester City kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya.
0 comments:
Post a Comment