 |
Arsen Wenger. |
Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameanza kupata hofu ya kutopata ile nafasi yake aliyoizoea, Wenger amezungumza na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa kwa sasa anapata hofu sana anapoona kuna uwezekanao wa timu yake kukosa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na mpaka hivi sasa Arsenal wapo nafasi ya nne huku wakiwa na pointi tano juu ya Manchester United ambao wana mchezo mmoja mkononi. Arsenal watacheza na timu ngumu inayotaka kushuka daraja Norwich City tarehe 30 na inategemewa kuwa mechi ngumu zaidi kwa Arsenal ambayo kwa sasa ni kama imepoteza muelekeo inapocheza na timu za mkiani.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment