Conte kuanza na Stones.
-Imefahamika kuwa kocha mpya wa klabu ya Chelsea Antonio Conte ataanza usajili wake kwa kumfukuzia kinda wa timu ya taifa ya England na klabu ya Everton John Stones. John Stones mwenye miaka 23 atakuwa ndiye mchezaji namba moja kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa darajani hapo mwezi wa sita dirisha la usajili litakapofunguliwa, thamani ya Stones kwa sasa inakadiriwa kuwa kiasi cha paundi milioni 37, Pia Stones anaangaliwa kama mrithi sahihi wa John Terry anayejiandaa kuachana na klabu hiyo ya darajani mwishoni mwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment