Ronaldo rasmi nje kuivaa Rayo,Pia hatihati kuivaaa Manchester City.


Real Madrid imetoa taarifa mchana huu kuhusiana na vipimo alivyofanyiwa mshambuliaji wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo na majibu yake yamekuwa sio mazuri sana japokuwa kuna matumaini. Majibu ya vipimo yanaonyesha Ronaldo aliumia nyama za nyuma za paja kwenye mechi ya juzi dhidi ya Villareal na kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuwa nje ya uwanja kwa mechi kadhaa zijazo. Zidane amesema bado haijajulikana ni muda gani nyota wake huyo atakuwa nje lakini mashabiki wafahamu kuwa hawatamuona Ronaldo uwanjani siku ya Jumamosi dhidi ya klabu ya Rayo Vallecao na pia haijajulikana kama atakuwa fiti kuwavaa Manchester City siku ya Jumanne kwenye dimba lao la Etihad kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya (UEFA).
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment