Henry amuhimiza Wenger kumsajili huyu kiungo.


Gwiji wa Arsenal Thierry Henry amesema kama kweli Wenger anataka mabadiliko msimu ujao ni lazima awe na kiungo aina N`Golo Kante wa klabu ya Leicester City. Henry akiongea na kituo cha television cha Sky sports alisema haoni sababu ya Wenger kutomsajili mchezaji mahiri kama Kante, kwanza ni mdogo halafu anacheza mpira wa akili huku pia akistahimili soka la kutumia nguvu, Pia Henry amesema Wenger anahitaji world class striker yaani mshambuliaji wa kiwango cha dunia ili aweze kutumia nafasi zinazotengenezwa na kiungo mahiri wa klabu hiyo Mesut Ozil. Arsenal kesho watakuwa uwanjani wakiumana na klabu ya Sunderland kwenye mchezo wa ligi.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment