 |
Mauro Icardi. |
Manchester United imekuwa ikimfuatilia mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan Mauro Icardi na ikawa inakumbana na wakati mgumu kwa kuwa Inter ilikonekana kurudi katika hali yake ya ushindi lakini hivi sasa mambo yamekuwa ndivyo sivyo kwa kuwa hakuna dalili za Inter Milan kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao na hilo ndilo jambo linalomfanya Icardi aondeke katika klabu hiyo. Icardi amesema alienda Inter Milan ili ashinde makombe pamoja na kushiriki kwenye mashindano yote makubwa lakini kama mambo hayatakuwa kama alivyopanga basi ataondoka zake, Hiyo ni taarifa njema kwa klabu ya Manchester United ambayo imekuwa ikimfuatilia mshambuliaji huyo kwa muda sasa.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment