Mama yake na Cristiano Ronaldo atoa ufafanuzi kuhusu mtoto wa pili wa Ronaldo.

Cristiano Ronaldo.
Mama yake na mshambuliaji hatari duniani na aliyetwaa tuzo ya Ballon d`Or mara tatu Cristiano Ronaldo ametolea ufafanuzi tetesi zilizotolewa na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu Ronaldo kutarajia  mtoto wa pili. Mama huyo aitwaye Dolores Aveiro amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa Ronaldo hana mpango wa kupata mtoto wa pili kwa sasa na ameziita taarifa hizo kuwa ni za uongo na hazina ukweli wowote. Cristiano Ronaldo ana mtoto mmoja aitwaye Cristiano Jr aliyezaliwa huko Marekani mwaka 2010 na mama yake bado hajawekwa hadharani mpaka sasa. Tetesi za Ronaldo kutarajia mtoto wa pili zilikuja baada ya kuwafunga Celta Vigo mwezi March na kushangilia akiwa ameweka mpira tumboni kitu ambacho huwa kinafanywa na wachezaji wengi pindi wapenzi wao wanapokuwa wajawazito.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment