Manchester United ipo mbioni kumaliza usajili wa Sanches.
-Gazeti la Daily Mail siku ya leo limetoa ripoti kuhusu sakata la usajili wa kiungo wa klabu ya Benfica Renato Sanches, Daily mail limesema klabu ya Manchester United ipo mbioni kumaliza usajili huo kabla ya michuano ya Euro haijaanza na watafanikisha dili hilo kwa kiasi cha paundi milioni arobaini na sita (£46 million) na watazilipa kwa mafungu kama ifuatavyo, kwanza watatanguliza paundi milioni 31 na baadae watamalizia kiasi cha paundi milioni 15 kwa ajili ya kumnasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18.
0 comments:
Post a Comment