 |
Yaya Toure. |
Taarifa za ndani ya klabu ya Manchester City zinaeleza kuwa katika mchezo wa leo wa nusu fainali ya kwanza ya klabu bingwa ya Ulaya Manchester City haitakuwa na kiungo wake mahiri na wa muhimu Yaya Toure kutokana na maumivu aliyoyapata wakati wa mechi dhidi ya Stoke na wakati wa mazoezi. Yaya Toure atakosa mchezo huu wa kwanza lakini anatarajiwa kuwa fiti kwa mchezo wa pili hapo mwezi ujao utakaopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu, Nafasi ya Toure leo inatazamiwa kuzibwa na wachezaji wawili (Fernandinho na Fernando). Manchester City leo inapambana na Real Madrid kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu yao.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment