Cristiano Ronaldo arudi kuwavaa Manchester City.



Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo ameanza mazoezi rasmi siku ya jana na ameungana rasmi na klabu yake na anatarajiwa kuwa fiti siku ya Jumatano ambapo klabu yake itapambana na klabu ya Manchester City katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa wa ulaya katika dimba la Santiago Bernabeu. Cristiano Ronaldo amekuwa nje kwa muda wa takribani wiki mbili na amekwisha kukosa michezo mitatu mmoja ukiwa wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Manchester City. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa nyota huyo anaendelea vizuri na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji kumi na moja watakaowavaa Manchester City.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment