Zidane amhofia Cristiano Ronaldo.
-Kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid amezungumza na waandishi wa habari baada ya kushinda mchezo wa jana dhidi ya Villareal, Real Madrid ilishinda mabao matatu kwa sifuri huku mabao yao yakifungwa na Karim Benzema, Lucas Vasquez na Luca Modrich, mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu ilimshuhudia nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo akitoka na maumivu ya misuli na kumpa kocha wake wasiwasi mkubwa. Zidane anasema wachezaji aina ya Ronaldo wanapaswa kupewa mapumziko na anajilaumu sana kwa nini hakumpumzisha nyota huyo ambaye bado haijajulikana ni kiasi gani maumivu hayo yanaweza kumuweka nje ya uwanja japokuwa Zidane anasema alipomuona kwenye vyumba vya kubadilishia nguo inaonekana yupo sawa sio tatizo kubwa na anasubiri vipimo vya madaktari siku ya leo.
0 comments:
Post a Comment