Wenger akataa kukanusha kuhusu Mahrez.

Riyad Mahrez.
Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal akiongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita amezungumzia kuhusu mambo mengi kuhusu mustakabali wa klabu yake haswa kipindi hiki kigumu kwa klabu hiyo baada ya kupoteza nafasi nyingine ya kunyanyua ubingwa wa England, Wenger ameulizwa na mwandishi mmoja wa habari kuhusu tetesi zilizosambaa wiki hii zikimuhusisha kiungo mshambuliaji wa klabu ya Leicester City Riyad Mahrez kutakiwa na Arsenal, Wenger amesema hawezi kukanusha taarifa hizo ila pia hawezi kuzizungumzia kwa sasa kwa kuwa itakuwa sio jambo la heshima kwa klabu ya Leicester City. Pia Wenger amesema nyota wake wawili Mesut Ozil na Alexis Sanchez wataendelea kuwepo klabuni hapo kwa kuwa bado mikataba yao haijaisha.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment