Wenger amvuruga Sanchez.

Arsen Wenger.
Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal Arsen Wenger ameonekana kumvuruga nyota wake kutoka Chile Alexis Sanchez, Wenger alimtoa Alexis nje ya uwanja katika dakika ya 83 katika mchezo wa juzi dhidi ya Norwich City ambao Arsenal walifanikiwa kushinda bao moja kwa sifuri. Wenger alipofanya tukio hilo, Sanchez alionekana kukerwa na kitendo hicho kiasi cha kumfanya kushindwa kuendelea kukaa uwanjani na kuamua kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo moja kwa moja, Sanchez anafahamika kwa kutokupenda kutolewa uwanjani na Wenger alipoulizwa kuhusu tukio hilo alijibu kwa kusema, najua Sanchez hafurahishwi kutolewa uwanjani lakini mimi ni mtu ninayetakiwa kuwapa watu wote raha na pale nilipofanya maamuzi ilikuwa ni kwa maslahi ya kulinda ushindi wa timu na sioni kama kuna kosa hapo.
Share on Google Plus

About Kings

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment